Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 28

Al-An'aam 6:28

الأنعام

بَلْ بَدَا لَهُم مَّا كَانُوا۟ يُخْفُونَ مِن قَبْلُ ۖ وَلَوْ رُدُّوا۟ لَعَادُوا۟ لِمَا نُهُوا۟ عَنْهُ وَإِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ

Maana

Bali yamewadhihirikia yale waliyokuwa wakiyaficha zamani. Na lau wangelirudishwa, bila ya shaka wangeliyarejea yale yale waliyokatazwa. Na hakika wao ni waongo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Bali yamewadhihirikia waliyo kuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangeli rudishwa bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyo katazwa. Na hakika hao ni waongo. [28]

[28] Na kauli yao hii haikuwa ila kwa kuwa haimkiniki tena kuficha wala kufanya ukaidi katika yale anayo waambia Mtume. Na lau kama wakirudishwa duniani wataurejea tena ukafiri alio wakataza Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa ghururi zao kughurika na mapambo ya dunia, na kwa kufuata kwao matamanio yao. Na hakika hao wanasema uwongo kwa kudai kuwa wataamini pindi wakirejeshwa duniani.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mambo si kama hivyo! Bali Siku ya Kiyama yatawadhihirikia wao yale waliokuwa wakiyafanya kwa nafsi zao, ya kuamini ukweli wa yale ambayo Mitume walikuja nayo ulimwenguni, ingawa walikuwa wakiwadhihirishia wafuasi wao kinyume chake. Na lau ingekadiriwa warudishwe ulimwenguni na waongezewe muda, wangalirudi kwenye upinzani kwa kukufuru na kukanusha. Na kwa kweli wao ni warongo katika neno lao, «Lau tutarudishwa ulimwenguni hatungalizikanusha aya za Mola wetu na tungalikuwa Waumini».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net