Al-An'aam 6:27
الأنعاموَلَوْ تَرَىٰٓ إِذْ وُقِفُوا۟ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُوا۟ يَـٰلَيْتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَـٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلْمُؤْمِنِينَ
Na lau ungeona waliposimamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungelirudishwa, wala tusizikadhibishe tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tuwe miongoni mwa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini. [27]
[27] Ewe Nabii! Lau ungeli waona hawa makafiri, watavyo simama mbele ya Moto wakisononeka na vitisho vyake, ungeli ona jambo la ajabu lenye kutisha, nao wanatamani warejeshwe tena duniani, wakisema: Laiti tungeli rudishwa duniani tukatengeneza tuliyo yaharibu! Wala hatutakanusha Ishara za Mola wetu Mlezi. Na tutakuwa miongoni wa Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na lau utawaona, ewe Mtume, washirikina hawa Siku ya Kiyama, utaona jambo kubwa, nalo ni wakati wao watakapofungwa juu ya Moto, na watakaposhuhudia yaliyomo humo miongoni mwa minyororo na pingu, na kujionea kwa macho yao mambo makubwa hayo na vituko hivyo. Hapo watasema, «Twatamani turudishwe kwenye maisha ya kilimwengu, tupate kuziamini aya za Allah Mtukufu na tuzitumie na tuwe ni miongoni mwa Waumini».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net