Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 26

Al-An'aam 6:26

الأنعام

وَهُمْ يَنْهَوْنَ عَنْهُ وَيَنْـَٔوْنَ عَنْهُ ۖ وَإِن يُهْلِكُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ

Maana

Nao huwazuia watu hayo, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi isipokuwa nafsi zao tu, wala wao hawatambui.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Nao huwazuia watu, na wao wenyewe wanajitenga nayo. Nao hawaangamizi ila nafsi zao tu, wala wao hawatambui. [26]

[26] Wao huwazuia watu wasiiamini Qur'ani, na wao wenyewe hujitenga nayo. Inakuwa wao hawanafiiki, wala hawawachii wenginewe wakanafiika! Na kwa kitendo hicho hawadhuru ila nafsi zao, na wao hawatambui ubaya wa wayatendayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na washirikina hawa wanawakataza watu kumfuata Mtume Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) na kumsikiliza, na wao wenyewe wanajiepusha naye. Na wao hawamuangamizi yoyote, kwa kuzuia kwao njia ya Allah Mtukufu isifuatwe, isipokuwa nafsi zao wenyewe, na wao hawatambui kuwa wajishughulisha na mambo ya kuzitia kwenye maangamivu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net