Al-An'aam 6:25
الأنعاموَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُ إِلَيْكَ ۖ وَجَعَلْنَا عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ أَكِنَّةً أَن يَفْقَهُوهُ وَفِىٓ ءَاذَانِهِمْ وَقْرًا ۚ وَإِن يَرَوْا۟ كُلَّ ءَايَةٍ لَّا يُؤْمِنُوا۟ بِهَا ۚ حَتَّىٰٓ إِذَا جَآءُوكَ يُجَـٰدِلُونَكَ يَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Na miongoni mwao kuna wale wanaokusikiliza; na tumezitia pazia kwenye nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi katika masikio yao, na wakiona kila Ishara, hawaiamini. Mpaka wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema wale waliokufuru: Hizi si chochote isipokuwa hadithi za watu wa kale.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza; na tumezitia pazia nyoyo zao wasije kuyafahamu. Na upo uziwi masikioni mwao, na wakiona kila Ishara hawaiamini. Hata wakikujia kwa kujadiliana nawe, wanasema walio kufuru: Hizi si chochote ila hadithi za watu wa kale. [25]
[25] Na miongoni mwao wapo wanao kusikiliza unapo soma Qur'ani, si kwa sababu waifahamu na ipate kuwaongoa, lakini ni kwa ajili wapate njia ya kuitoa kombo na kuikejeli. Na Sisi kwa sababu hiyo tumewazuilia wasiweze kunafiika kwa akili zao na masikio yao. Imekuwa kama kwamba akili zao zimefunikwa haziwezi kuelewa baraabara; na kama kwamba masikio yao yana uziwi unao wazuia wasizisikie Aya za Qur'ani. Na hawa hata wakiona kila dalili hawaamini. Hata wakikujia wakujadili kwa upotovu wanasema walio kufuru, huku wakisukumiza na ukafiri wao: Haya si chochote ila hadithi za uwongo zilizo tungwa na watu wa zamani wa kabla yako!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kati ya washirikina hawa kuna wanaokusikiliza usomapo Qur’ani, ewe Mtume, na isifike kwenye nyoyo zao. Kwa kuwa wao, kwa sababu ya kufuata matamanio yao, tumeweka vifuniko juu ya nyoyo zao wasipate kuifahamu Qur’ani. Na tumejaalia kwenye masikio yao uzito na uziwi, hayasikii wala hayafahamu chochote. Na wanapoziona dalili nyingi zenye kuonyesha ukweli wa Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) hawaziamini. Na hata wakikujia, ewe Mtume, baada ya kuzishuhudia dalili zenye kuonesha ukweli wako, huwa wakisema wenye kuzikanusha aya za Allah Mtukufu, «Haya tunayoyasikia si chochote isipokuwa ni ngano zinazohadithiwa na watu wa kale zisizo na ukweli».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net