Al-An'aam 6:24
الأنعامٱنظُرْ كَيْفَ كَذَبُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ ۚ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا۟ يَفْتَرُونَ
Tazama jinsi wanavyosema uongo juu ya nafsi zao wenyewe. Na yamewapotea waliyokuwa wakiyazua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tazama jinsi wanavyo jisemea uwongo wenyewe. Na yamewapotea waliyo kuwa wakiyazua. [24]
[24] Angalia vipi wanavyo jitia makosani wenyewe kwa uwongo huu. Na vile walivyo kuwa wameviunda wenyewe kwa kuviabudu, navyo ni mawe tu, na wakadai kuwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu, sasa vimewapotea
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Fikiri, ewe Mtume, vipi washirikina hawa wanasema urongo juu ya nafsi zao, na wao kesho Akhera watajiepusha na ushirikina! Yatawaondokea wao na kuwapotea yale waliokuwa wakiyadhania ya kuwa waungu wao watawaombea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net