Al-An'aam 6:23
الأنعامثُمَّ لَمْ تَكُن فِتْنَتُهُمْ إِلَّآ أَن قَالُوا۟ وَٱللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشْرِكِينَ
Kisha hautakuwa udhuru wao isipokuwa ni kusema: Wallahi (Tunaapa kwa Mwenyezi Mungu), Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha hautakuwa udhuru wao ila ni kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina. [23]
[23] Kisha hayatakuwa matokeo ya hayo matatizo yao magumu pahala hapo ila kujitoa kimaso-maso kutokana na ushirikina wao kwa kusema uwongo. Waseme: Wallahi Mola Mlezi wetu! Hatukumshirikisha nawe yeyote katika ibada.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha hayakuwa majibu yao, walipojaribiwa na kupewa mtihani kwa kuulizwa kuhusu washirika wao, isipokuwa walijitoa na wao na wakaapa kwamba wao hawakuwa ni wenye kumshirikisha yoyote na Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net