Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 22

Al-An'aam 6:22

الأنعام

وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوٓا۟ أَيْنَ شُرَكَآؤُكُمُ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ

Maana

Siku tutakapowakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie wale walioshirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mliokuwa mkidai?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio shirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai? [22]

[22] Na watajie yatakayo tokea Siku tutapo kusanya viumbe vyote kwa ajili ya hisabu. Kisha tutawaambia kwa kuwahizi walio kuwa wakiwaabudu wenginewe pamoja na Mwenyezi Mungu: Wako wapi mlio wafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu, wapate kukufaeni?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wajihadhari washirikina hawa wenye kuzikanusha aya za Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na Siku ambayo tutawafufua kisha tutasema kuwaambia, «Wako wapi waungu wenu ambao mlikuwa mkidai kuwa wao ni washirika na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ili wawaombee nyinyi?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net