Al-An'aam 6:21
الأنعاموَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِـَٔايَـٰتِهِۦٓ ۗ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ
Na nani dhalimu zaidi kuliko anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu, au akazikadhibisha Ishara zake? Hakika madhalimu hawafaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi. [21]
[21] Na hapana mtu aliye zidi kuidhulumu nafsi yake na Haki, kuliko anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, na akadai kuwa Yeye Subhanahu ana mwana au mshirika, au akamwambatisha lolote lisilo laiki yake, au akazikanya dalili zenye kuonyesha Umoja wake Mwenyezi Mungu na ukweli wa Mitume wake. Hakika madhaalimu hawatopata kheri duniani wala Akhera.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote mwenye udhalimu mbaya zaidi kuliko yule aliyemzulia Allah Mtukufu, Aliyetukuka, urongo na akadai kwamba Yeye Ana washirika katika ibada, au akadai kwamba Yeye Ana mtoto au mke, au akazikanusha hoja Zake na dalili ambazo kwazo Aliwapa nguvu Mitume Wake, amani iwashukie. Hakika ya mambo ni kwamba madhalimu waliomzulia Allah Mtukufu urongo hawafaulu na hawapati matakwa yao ulimwenguni wala Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net