Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 20

Al-An'aam 6:20

الأنعام

ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَعْرِفُونَهُۥ كَمَا يَعْرِفُونَ أَبْنَآءَهُمُ ۘ ٱلَّذِينَ خَسِرُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ فَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ

Maana

Wale tuliowapa Kitabu wanakijua kama wanavyowajua watoto wao. Wale waliozihasiri nafsi zao, basi wao hawaamini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale Tulio wapa Kitabu wanayajua haya kama wanavyo wajua watoto wao. Wale walio zikhasiri nafsi zao hawaamini. [20]

[20] Tulio wapa Vitabu vya mbinguni, Mayahudi na Wakristo, wanamjua vyema Muhammad na ukweli wa Utume wake kutokana na hivyo Vitabu vyao vya Biblia, kama wanavyo wajua watoto wao. Walio zipoteza nafsi zao hawayakubali yale wanayo yajua. Kwa hivyo hao hawaamini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale tuliowapa Taurati na Injili wanamjua Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) kwa sifa Zake zilizoandikwa kwao kama wanavyowajua watoto wao. Na kama ilivyo wao hawachanganyikiwi kuwajua watoto wao walio mbele yao kuwapambanua na wengine, vilevile Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) hachanganyiki na mwingine, kwa sababu ya uwazi wa sifa zake zilizo ndani ya vitabu vyao. Lakini wao walifuata matamanio yao, walipomkanusha Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,) na yale aliyokuja nayo, ndipo wakapata hasara nafsi zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net