Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 21

وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِـَٔايَـٰتِهِۦٓ ۗ إِنَّهُۥ لَا يُفْلِحُ ٱلظَّـٰلِمُونَ 21

{21} Yaani, hakuna kubwa zaidi katika dhuluma na ukaidi kuliko yule ambaye ana sifa moja kati ya mbili hizi. Basi itakuwaje zikijumuika, kumsingizia Mwenyezi Mungu uwongo, au kuzikadhibisha Ishara zake ambazo walikuja nazo Mitume? Basi huyu hakika ndiye dhalimu zaidi miongoni mwa watu. Na dhalimu hafaulu kamwe. Na anaingia katika hili kila mwenye kumsingizia uongo Mwenyezi Mungu kwa kudai kuwa Mwenyezi Mungu ana mshirika na msaidizi; au anayedai kwamba anafaa kuabudiwa asiyekuwa Yeye; au alimfanya kuwa na mke; au mtoto, na kila mwenye kuikataa haki ambayo walikuja nayo Mitume au mwenye kusimama mahali pao.