Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 155

Al-An'aam 6:155

الأنعام

وَهَـٰذَا كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ مُبَارَكٌ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُوا۟ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

Maana

Na hiki ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa. Basi kifuateni, na mcheni, ili mrehemewe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha, kilicho barikiwa. Basi kifuateni, na mchenimngu, ili mrehemewe. [155]

[155] Na hii Qur'ani ni Kitabu, kilicho barikiwa, tulicho kiteremsha, chenye kukusanya kheri za Mwenyezi Mungu, na manufaa ya Dini na dunia. Basi kifuateni, na ogopeni msende kinyume chake, ili Mola wenu Mlezi apate kukurehemuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na hii Qur’ani ni kitabu tulichokiteremsha kwa Nabii wetu Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie.) Kheri zake ni nyingi. Basi kifuateni kwa yale anayowaamrisha na kuwakataza. Na muogopeni Allah Mtukufu msije mkaenda kinyume na amri Yake yoyote, kwa matumaini kuwa mtarehemewa na mtaokolewa na adhabu Yake na mpate malipo Yake mema.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net