Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-An'aam
Sura ya 6

Al-An'aam

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 155

وَهَـٰذَا كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ مُبَارَكٌ فَٱتَّبِعُوهُ وَٱتَّقُوا۟ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ 155

{155} "Na hiki" yaani Qur-aani hii Tukufu, na ukumbusho wenye hekima "ni Kitabu tulichokiteremsha, kilichobarikiwa." Yaani, ndani yake kuna kheri nyingi na elimu tele, nayo ndiyo ambayo zinatolewa elimu nyinginezo zote, zinatolewa humo baraka. Basi hakuna kheri yoyote isipokuwa iliita kwayo na ilitia moyo wa kuiendea, na ikataja hekima mbalimbali na maslahi ambayo yanahimiza juu yake. Na hakuna uovu wowote isipokuwa iliukataza na kuonya dhidi yake, na ikataja sababu za kujitenga na kuufanya na matokeo yake mabaya. "Basi kifuateni" katika yale inayoyaamrisha na kuyakataza. Na jengeni misingi ya dini yenu na matawi yake juu yake. "Na mcheni" Mwenyezi Mungu Mtukufu mkaja mkahalifu amri yake yoyote "ili" mkiifuata "mrehemewe." Basi sababu kubwa zaidi ya kupata rehema ya Mwenyezi Mungu ni kukifuata kitabu hiki kwa elimu na vitendo.