Al-An'aam 6:154
الأنعامثُمَّ ءَاتَيْنَا مُوسَى ٱلْكِتَـٰبَ تَمَامًا عَلَى ٱلَّذِىٓ أَحْسَنَ وَتَفْصِيلًا لِّكُلِّ شَىْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُم بِلِقَآءِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) yule aliyefanya uzuri, na kuwa ni maelezo ya kina ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili waamini katika kukutana na Mola wao Mlezi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tena tulimpa Musa Kitabu kwa kumtimizia (neema) aliye fanya wema, na kuwa ni maelezo ya kila kitu, na uwongofu na rehema, ili wapate kuamini mkutano wao na Mola wao Mlezi. [154]
[154] Na tulimteremshia Musa Taurati kwa kumtimizia neema mtu aliye simama msimamo mwema katika mambo ya Dini. Na tuliiteremsha kwa kueleza wazi kila jambo katika mafunzo yalio nasibiana na watu wake, na ni uwongofu kwendea Njia iliyo sawa, na rehema kwao kwa kuifuata. Na hayo ni hivyo ili Wana wa Israili waiamini Siku ya kukutana na Mola wao Mlezi, Siku ya Kiyama na kuhisabiwa kwa mambo walio amrishwa kuyafanya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha sema, ewe Mtume, uwaambie hawa washirikina, Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Ndiye Aliyempa Mûsã Taurati, kwa kuzitimiza neema Zake kwa watu wa mila yake wanaofanya wema, na kwa kufafanua kila kitu katika mambo ya dini yao, na kuwapa uongofu na muelekeo wa njia iliyolingana sawa, na kuwarehemu, kwa matumaini kuwa watakubali kwamba kuna kufufuliwa baada ya kufa na kuna hesabu na malipo, na hilo liwafanye watende mema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net