Al-An'aam 6:153
الأنعاموَأَنَّ هَـٰذَا صِرَٰطِى مُسْتَقِيمًا فَٱتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا۟ ٱلسُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِۦ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّىٰكُم بِهِۦ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ
Na kwamba hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Wala msifuate njia nyinginezo, zikakutengeni mbali na Njia yake. Haya amewausia ili mche (Mwenyezi Mungu).
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu. [153]
[153] Wala msiiache Njia niliyo kuwekeeni, kwani hiyo ndiyo Njia Iliyo Nyooka itayo kufikisheni kwenye mafanikio ya duniani na Akhera. Bali ifuateni Njia hii, wala msifuate njia nyingine za upotovu alizo kukatazeni Mwenyezi Mungu, ili msije kufarikiana mkawa makundi makundi na mapande mapande, ya madhehebu na vyama, na mkawa mbali na Njia ya Mwenyezi Mungu iliyo kaa sawa. Mwenyezi Mungu amekuamrisheni kwa amri ya nguvu ili msije mkamkhalifu Yeye.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa mambo aliyowausia Allah Mtukufu ni kwamba huu Uislamu ndio njia ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka, iliyolingana sawa. Basi ifuateni wala msifuate njia za upotevu zikawatawanya na kuwaepusha na njia ya Allah Mtukufu iliyolingana sawa. Muelekeo huo upande wa njia nyofu, ndio Aliowausia nao Allah Mtukufu ili mjikinge na adhabu Yake kwa kuyatekeleza maamrisho Yake na kijitenga na makatazo Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net