Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 6 · Aya ya 156

Al-An'aam 6:156

الأنعام

أَن تَقُولُوٓا۟ إِنَّمَآ أُنزِلَ ٱلْكِتَـٰبُ عَلَىٰ طَآئِفَتَيْنِ مِن قَبْلِنَا وَإِن كُنَّا عَن دِرَاسَتِهِمْ لَغَـٰفِلِينَ

Maana

Mkaja kusema, “Hakika waliteremshiwa Kitabu makundi mawili tu kabla yetu, na sisi tulikuwa hatuna habari ya waliyokuwa wakiyasoma.”

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Msije mkasema: Hakika mataifa mawili kabla yetu yameteremshiwa Kitabu; na sisi tulikuwa hatuna khabari ya waliyo kuwa wakiyasoma. [156]

[156] Tumeiteremsha hii Qur'ani ili msipate kutoa udhuru kwa uasi wenu mkasema: Wahyi haukuteremka ila kwa mataifa mawili tu ya kabla yetu, nao ni watu wa Taurati na watu wa Injili. Na sisi hatuna ilimu kabisa ya kusoma vitabu vyao na kufahamu uwongozi uliomo humo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na tumeiteremsha hii Qur’ani, ili msije mkasema, enyi makafiri wa Kiarabu, «Hakika Kitabu kutoka mbinguni waliteremshiwa Mayahudi na Wanaswara; na sisi tuna mambo ya kutushughulisha kutowahi kuvisoma vitabu vyao; na sisi hatuna ujuzi navyo wala maarifa».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-An'aam

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net