Al-Hashr 59:7
الحشرمَّآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنْ أَهْلِ ٱلْقُرَىٰ فَلِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ وَلِذِى ٱلْقُرْبَىٰ وَٱلْيَتَـٰمَىٰ وَٱلْمَسَـٰكِينِ وَٱبْنِ ٱلسَّبِيلِ كَىْ لَا يَكُونَ دُولَةًۢ بَيْنَ ٱلْأَغْنِيَآءِ مِنكُمْ ۚ وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟ ۚ وَٱتَّقُوا۟ ٱللَّهَ ۖ إِنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ
Mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili isiwe ikizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anachokupeni Mtume, kichukueni. Na anachokukatazeni, jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu. [7]
[7] Alicho rudisha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake katika mali ya watu wa vijiji hivi bila ya kuwatimua farasi au ngamia, vitu hivyo ni vya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri. Haya ni hivyo ili yasiwe mali yakizunguka katika mikono ya matajiri peke yao katika nyinyi. Na anacho kupeni Mtume katika hukumu basi kishikeni, na anacho kukatazeni basi kiwacheni. Na jilindeni na kughadhibika kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hiyo mali ya washirikina wa watu wa miji ambayo Allah Mtukufu Amewaletea bila kupanda farasi wala ngamia, basi hiyo ni ya Allah Mtukufu na ya Mtume Wake, itatumiwa kwa maslahi ya Waislamu kwa jumla, jamaa wa karibu wa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na mayatima: nao ni «watoto maskini waliofiliwa na baba zao, maskini: nao ni wenye uhitaji na ufukara, na ibn al- sabīl: naye ni mgeni msafiri ambaye matumizi yake yameisha na mali yake imemalizika». Hiyo ni kwa sababu mali isiwe ni milki inayozunguka kwa matajiri peke yao, na mafukara na maskini wakanyimwa nayo. Na mali yoyote ambayo Mtume Amewapatia, au sheria yoyote aliyowawekea, basi chukueni, na chochote kile alichowakataza basi komekeni nacho. Na muogopeni Allah Mtukufu kwa kufuata amri Zake na kuepuka makatazo Yake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwenye mateso makali kwa anayemuasi na kuenda kinyume na amri Yake na makatazo Yake. Na aya hii ni msingi wa ulazima wa kufuata Sunnah iwe ni ya maneno, ya vitendo au ya kukubali jambo lifanyike mbele ya mtume na kutolikataza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net