Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 6

Al-Hashr 59:6

الحشر

وَمَآ أَفَآءَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦ مِنْهُمْ فَمَآ أَوْجَفْتُمْ عَلَيْهِ مِنْ خَيْلٍ وَلَا رِكَابٍ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يُسَلِّطُ رُسُلَهُۥ عَلَىٰ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ

Maana

Na mali aliyoileta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuikimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza mno juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwao hamkuyakimbilia mbio kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa mamlaka Mitume wake juu ya wowote awatakao. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza juu ya kila kitu. [6]

[6] Na aliyo yaleta Mwenyezi Mungu na akayarudisha kwa Mtume wake katika mali ya Banu Nnadhir hamkuyapigia mbio nyinyi kwa farasi wala ngamia. Lakini Mwenyezi Mungu huwapa madaraka Mitume wake kwa awatakao katika waja wake bila ya kupigana vita. Na Mwenyezi Mungu ni Mtimilivu wa uweza juu ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na ile mali ya Mayahudi wa Banū al- Naḍīr ambayo Allah Mtukufu Amewaletea, hamkupanda farasi wala ngamia ili muipate, bali Allah Mtukufu Anawapa nguvu mitume Wake juu ya anayemtaka miongoni mwa maadui Wake, wakajisalimsha bila ya vita. (Mali hiyo inaitwa fay’), na fay’ ni mali iliyochukuliwa kutoka kwa makafiri kwa haki bila vita. Na Allah Mtukufu kwa kila jambo ni Muweza, hakuna kitu chochote kinachomshinda.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net