Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 5

Al-Hashr 59:5

الحشر

مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَآئِمَةً عَلَىٰٓ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ ٱللَّهِ وَلِيُخْزِىَ ٱلْفَـٰسِقِينَ

Maana

Mtende wowote mlioukata au mliouacha umesimama vile vile juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na ili awahizi wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mtende wowote mlio ukata au mlio uacha unasimama vile vile juu ya mashina yake, basi ni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kwa kuwahizi wapotovu. [5]

[5] Enyi Waislamu! Mitende yoyote mliyo ikata au mkaiacha imebaki kama ilivyo kuwa, basi ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hapana lawama juu yenu katika hayo, ili awape nguvu Waumini, na awahizi wapotovu walio ziacha sharia zake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mitende mnayoikata au mnayoiacha imesimama juu ya mashina yake bila ya kuigusa, ni kwa idhini ya Allah Mtukufu na amri Yake, na ili Awadhalilishe kwa hilo wale waliotoka nje ya utiifu Kwake wenye kuenda kinyume na amri Yake na makatazo Yake, kwa kuwapa nguvu nyinyi kuikata mitende yao na kuichoma.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net