Al-Hashr 59:8
الحشرلِلْفُقَرَآءِ ٱلْمُهَـٰجِرِينَ ٱلَّذِينَ أُخْرِجُوا۟ مِن دِيَـٰرِهِمْ وَأَمْوَٰلِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ ٱللَّهِ وَرِضْوَٰنًا وَيَنصُرُونَ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥٓ ۚ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصَّـٰدِقُونَ
Wapewe mafakiri Wahajiri waliotolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wakweli.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wapewe mafakiri Wahajiri walio tolewa majumbani mwao na mali yao kwa ajili ya kutafuta fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu na radhi zake, na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hao ndio wa kweli. [8]
[8] Na hivyo yale mali ya watu wa vijiji aliyo yarudisha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake wapewe mafakiri katika Wahajiri, walio kimbilia Madina, ambao wametolewa majumbani kwao na mali yao huko Makka. Wao wanataraji ziada kutoka kwa Mwenyezi Mungu katika riziki zao na radhi. Na wanamsaidia Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa nafsi zao na mali yao. Hao ndio Waumini wa kweli.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Pia wanapewa mali hiyo, ambayo Allah Mtukufu Amemletea Mtume Wake, mafukara waliohama, wale waliolazimishwa na makafiri wa Makkah watoke kwenye majumba yao na waache mali zao na huku wanaomba kwa Allah Mtukufu Awafanyie hisani ya kuwapa riziki duniani na radhi kesho Akhera, na wanaitetea Dini ya Allah Mtukufu na Mtume Wake kwa kupigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu. Hao ndio wakweli ambao walikuwa wakweli wa maneno yao na vitendo vyao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net