Al-Hashr 59:9
الحشروَٱلَّذِينَ تَبَوَّءُو ٱلدَّارَ وَٱلْإِيمَـٰنَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِى صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّآ أُوتُوا۟ وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْمُفْلِحُونَ
Na wale walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda wale waliohamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyopewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda walio hamia kwao, wala hawaoni choyo katika vifua vyao kwa walivyo pewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kuliko nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wahitaji. Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa. [9]
[9] Na Ma-ansari, watu wa Madina walio mnusuru Mtume na Wahajiri, ambao wamekaa Madina katika maskani zao, na Imani yao ikawa safi kabisa kabla ya kufika Wahajiri, wanawapenda wale wageni Waislamu walio hamia kwao, na wala hawahisi ubaya wowote katika nafsi zao kwa walicho pewa Wahajiri katika ngawira. Bali wanawakadimisha Wahajiri kuliko nafsi zao, ijapo kuwa wakiwa wao nao ni wahitaji. Na mwenye kuhifadhika, kwa uweza wa Mwenyezi Mungu, asione ubakhili katika nafsi yake, basi watu kama hao ndio wenye kufuzu kwa kila walipendalo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wale wakazi wa Madina na walioamini kabla ya Waumini wa Makkah hawajahamia Madina, nao ni Anṣār (Waumini wenyeji wa Madina) wanawapenda Muhājirūn (Waumini waliohamia Madina) na wanawaliwaza kwa mali zao, wala hawaoni wivu juu yao kwa mali ya fay’ waliyopewa, na wanawatanguliza waliohama na wenye uhitaji na ufukara juu ya nafsi zao, japokuwa wao wana uhitaji na ufukara. Na yoyote aliyesalimika na ubahili na uzuiaji wa mali iliyozidi, basi hao ndio wenye kufuzu, waliofaulu kupata matakwa yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net