Al-Hashr 59:10
الحشروَٱلَّذِينَ جَآءُو مِنۢ بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا ٱغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَٰنِنَا ٱلَّذِينَ سَبَقُونَا بِٱلْإِيمَـٰنِ وَلَا تَجْعَلْ فِى قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ رَبَّنَآ إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ
Na wale waliokuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu waliotutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walioamini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu mno.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kuja baada yao wanasema: Mola wetu Mlezi! Tughufirie sisi na ndugu zetu walio tutangulia kwa Imani, wala usijaalie ndani ya nyoyo zetu undani kwa walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe ni Mpole na Mwenye kurehemu. [10]
[10] Na Waumini walio kuja baada ya Wahajiri na Ansari husema: Mola wetu Mlezi! Tusamehe dhambi zetu, sisi na ndugu zetu walio tutangulia katika Imani. Wala usijaalie kuwa katika nyoyo zetu husda kuwahusudu walio amini. Mola wetu Mlezi! Hakika Wewe umefika ukomo katika upole na kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na waliokuja miongoni mwa Waumini baada ya Anṣār na Muhājirūn wanasema, «Mola wetu! Tusamehe dhambi zetu, na uwasamehe ndugu zetu katika Dini waliotutangulia katika kuamini, na usitie ndani ya nyoyo zetu uhasidi na chuki kwa yoyote miongoni mwa wenye kuamini. Mola wetu! Wewe ni Mpole kwa waja wako. Unawarehemu waja wako rehema pana katika maisha yao ya hapa ulimwenguni na ya kesho Akhera». Katika hii aya pana dalili kwamba inapasa kwa Muislamu awataje kwa wema wale waliomtangulia na awaombee dua, na awapende maswahaba wa Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na awataje kwa wema na awaombee radhi za Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net