Al-Hashr 59:11
الحشرأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ نَافَقُوا۟ يَقُولُونَ لِإِخْوَٰنِهِمُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْ أَهْلِ ٱلْكِتَـٰبِ لَئِنْ أُخْرِجْتُمْ لَنَخْرُجَنَّ مَعَكُمْ وَلَا نُطِيعُ فِيكُمْ أَحَدًا أَبَدًا وَإِن قُوتِلْتُمْ لَنَنصُرَنَّكُمْ وَٱللَّهُ يَشْهَدُ إِنَّهُمْ لَكَـٰذِبُونَ
Huwaoni wale wanaofanya unafiki wanawaambia ndugu zao waliokufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa, na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamtii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita, lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huwaoni wanao fanya unaafiki wanawaambia ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu: Mkitolewa na sisi lazima tutatoka pamoja nanyi, wala hatutamt'ii yeyote kabisa dhidi yenu. Na mkipigwa vita lazima tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hao hakika bila ya shaka ni waongo. [11]
[11] Hebu huwaangalii hao wanaafiki ukastaajabu? Kazi yao ni kuwakariria kauli ndugu zao walio kufuru katika Watu wa Kitabu - nao ni hao Banu Nnadhir - kuwaambia: Wallahi! Mkilazimishwa kuihama Madina, basi hapana shaka na sisi tutatoka pamoja nanyi. Wala hatutamt'ii katika jambo lenu mtu yeyote daima dawamu. Na pindi ikiwa Waislamu watakupigeni vita, basi hapana shaka sisi tutakusaidieni. Na Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa hakika wanaafiki hapana shaka ni waongo katika hizo ahadi zao wanazo zitoa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hivi huwaoni hao wanafiki wanaowaambia ndugu zao katika ukafiri miongoni mwa Mayahudi wa Banū al Naḍīr, «Tunaapa kwamba Muhammad na walio pamoja naye wakiwatoa kutoka majumbani mwenu tutatoka na nyinyi! Na hatutamfuata yoyote anayetutaka tusiwasaidie au tuache kutoka pamoja nanyi, na wakipigana na nyinyi tutawasaidia nyinyi juu yao?» na Allah Mtukufu Anashuhudia kwamba wanafiki ni warongo katika yale waliyowaahidi Banū al Naḍīr.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net