Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 12

Al-Hashr 59:12

الحشر

لَئِنْ أُخْرِجُوا۟ لَا يَخْرُجُونَ مَعَهُمْ وَلَئِن قُوتِلُوا۟ لَا يَنصُرُونَهُمْ وَلَئِن نَّصَرُوهُمْ لَيُوَلُّنَّ ٱلْأَدْبَـٰرَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ

Maana

Pindi wakitolewa, hawatatoka pamoja nao. Na wakipigwa vita, hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia, basi watageuza mno migongo; kisha hawatanusuriwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Pindi wakitolewa hawatatoka pamoja nao, na wakipigwa vita hawatawasaidia. Na kama wakiwasaidia basi watageuza migongo; kisha hawatanusuriwa. [12]

[12] Wakitolewa Mayahudi, wanaafiki hawatatoka pamoja nao. Na wakipigwa vita hawatawanusuru. Na pindi wakiwasaidia basi hapana shaka watatoka mbio warudi kinyume nyume, wala hawatawanusuru.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau Mayahudi watatolewa Madina, wanafiki hawatatoka pamoja nao, na lau watapigwa vita hawatapigana pamoja nao kama walivyoahidi. Na lau watapigana pamoja nao watakimbia kukimbia kwa kushindwa, kisha Allah Mtukufu Hatawanusuru, bali Atawaacha bila kuwasaidia na Atawadhalilisha.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net