Al-Hashr 59:13
الحشرلَأَنتُمْ أَشَدُّ رَهْبَةً فِى صُدُورِهِم مِّنَ ٱللَّهِ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَفْقَهُونَ
Hakika nyinyi ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasiofahamu kitu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika nyinyi ni kitisho zaidi katika vifua vyao kuliko Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa kuwa hao ni watu wasio fahamu kitu. [13]
[13] Hakika, enyi Waislamu, mna kitisho zaidi katika vifua vya wanaafiki na Mayahudi kuliko wanavyo mwogopa Mwenyezi Mungu. Hayo ni kwa sababu hakika wao ni watu wasio jua ukweli wa Imani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, hofu ya wanafiki na Mayahudi kuwaogopa nyinyi, (enyi Waumini), ni kubwa mno ndani ya nyoyo zao kuliko vile wanavyomuogopa Allah Mtukufu. Hii ni kwa sababu ya kuwa wao ni watu wasiouelewa utukufu wa Allah Mtukufu na kuwa na Imani Kwake, na hawaogopi mateso Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net