Al-Hashr 59:14
الحشرلَا يُقَـٰتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِى قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَآءِ جُدُرٍۭ ۚ بَأْسُهُم بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ ۚ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ
Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipokuwa katika vijiji vilivyoimarishwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasiotumia akili.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili. [14]
[14] Mayahudi hawapigani vita nanyi kwa pamoja ila wawe katika miji iliyo jengewa ngome, au wajifiche nyuma ya kuta. Vita vyao baina ya wao kwa wao ni vikali. Utawadhani kuwa wameshikamana, wote ni wamoja. Kumbe hakika nyoyo zao zimefarikiana mbali mbali. Wao ni wenye sifa hizo, kwa sababu hao ni watu wasio zingatia nini utakuwa mwisho wa mambo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hawatakabiliana na nyinyi (Mayahudi) wakiwa wamejikusanya isipokuwa wakiwa kwenye miji iliyohifadhiwa kwa ngome na mahandaki, au nyuma ya kuta ambazo wanazitumia kwa kujificha kwa uoga wao uliojikita ndani ya nyoyo zao. Uadui baina yao ni mkubwa, utadhani wamekusanyika kwenye neno moja, lakini nyoyo zao ziko mbalimbali, na hiyo ni kwa sababu wao ni watu wasioitia akilini amri ya Allah Mtukufu wala kuzizingatia aya Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net