Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 15

Al-Hashr 59:15

الحشر

كَمَثَلِ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ قَرِيبًا ۖ ذَاقُوا۟ وَبَالَ أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

Maana

Ni kama mfano wa wale waliokuwa kabla yao hivi karibuni, walionja uovu wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni kama mfano wa walio kuwa kabla yao hivi karibuni. Walionja uovu wa mambo yao. Nao watapata adhabu iliyo chungu. [15]

[15] Mfano wa Bani Nnadhir ni kama mfano wa walio kufuru kabla yao karibuni. Hao walionja hapa hapa duniani matokeo ya ukafiri wao na kuvunja kwao mapatano. Na Akhera watapata adhabu ya uchungu mkali.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mfano wa hawa Mayahudi kwa mateso yaliyowashukia ni kama mfano wa makafiri wa kikureishi siku ya Badr na Mayahudi wa Banū Qaynuqā‛kwa kuwa walionja mwisho mbaya wa ukafiri wao na uadui wao kwa Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), duniani, na huko Akhera watapata adhabu kali yenye uchungu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net