Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 59 · Aya ya 16

Al-Hashr 59:16

الحشر

كَمَثَلِ ٱلشَّيْطَـٰنِ إِذْ قَالَ لِلْإِنسَـٰنِ ٱكْفُرْ فَلَمَّا كَفَرَ قَالَ إِنِّى بَرِىٓءٌ مِّنكَ إِنِّىٓ أَخَافُ ٱللَّهَ رَبَّ ٱلْعَـٰلَمِينَ

Maana

Ni kama mfano wa Shetani anapomwambia mtu: 'Kufuru.' Na akikufuru, humwambia: 'Hakika mimi niko mbali zaidi nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.'

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni kama mfano wa Shetani anapo mwambia mtu: Kufuru. Na akikufuru humwambia: Mimi si pamoja nawe. Hakika mimi namwogopa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote. [16]

[16] Mfano wa wanaafiki kuwashawishi Banu Nnadhir wamuasi Mtume wa Mwenyezi ni kama mfano wa Shetani pale anapo mghuri mtu aiache Imani, akamwambia: Kufuru! Na alipo kufuru akasema: Mimi niko mbali nawe, kwani mimi ninamkhofu Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa hawa wanafiki katika kule kuwashawishi Mayahudi wapigane na kuwaahidi kuwa watawatetea dhidi ya Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ni kama mfano wa Shetani alipompambia binadamu na kumlingania kwenye ukafiri, na alipokufuru alisema, «Mimi nimejitakasa na wewe; mimi namuogopa Allah Mtukufu Mola wa viumbe wote».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Hashr

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net