Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 79

Al-Maaida 5:79

المائدة

كَانُوا۟ لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ

Maana

Walikuwa hawakatazani maovu waliyokuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu mno waliyokuwa wakiyafanya!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walikuwa hawakatazani maovu waliyo kuwa wakiyafanya. Hakika ni maovu yalioje mambo waliyo kuwa wakiyafanya! [79]

[79] Mtindo wao ulikuwa kutoambizana. Hapana amkatazaye mwenzie kufanya uovu. Kufanya kwao uovu na kuacha kukatazana ni katika vitendo vinavyo chusha mno!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walikuwa, Mayahudi hawa, wakiyafanya maasia waziwazi, wakiridhika nayo na hawakuwa wakikatazana wao kwa wao maovu yoyote waliyoyafanya. Na hili ni katika vitendo vyao viovu. Na kwa hilo walistahiki kufukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net