Al-Maaida 5:78
المائدةلُعِنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنۢ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ عَلَىٰ لِسَانِ دَاوُۥدَ وَعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا۟ وَّكَانُوا۟ يَعْتَدُونَ
Walilaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapita mipaka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Walilaaniwa walio kufuru miongoni mwa Wana wa Israili kwa ulimi wa Daud na wa Isa mwana wa Maryamu. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakawa wanapindukia mipaka. [78]
[78] Mwenyezi Mungu amewatenga mbali na rehema yake wale makafiri miongoni mwa Wana wa Israili, na haya yameteremka katika Zaburi juu ya Nabii wake Daud, na katika Injili juu ya Nabii wake Isa mwana wa Maryam. Na hayo ni kwa sababu ya uasi wao, kutokana na ut'iifu wa Mwenyezi Mungu na kuzama kwao katika udhalimu na ufisadi.(Katika Zaburi Daud anawaapiza Mayahudi:"Wewe, Mungu, uwapatilize. Na waanguke kwa mashauri yao, Uwatoe nje kwa ajili ya wingi wa makosa yao, kwa maana wamekuasi Wewe." - Zaburi 5.10. Katika Injili Yesu anawalaani: "Enyi nyoka, wana wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?" - Mathayo 23.33.)
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anatoa habari kwamba Amewafukuza kutoka kwenye rehema Yake makafiri miongoni mwa Wana wa Isrãîl, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu ambacho Allah Mtukufu Alikiteremsha kwa Dãwûd, amani imshukie, nacho ni Zaburi, na kwenye kitabu Alichokiteremsha kwa ‘Ǐsâ, amani imshukie, nacho ni Injili, kwa sababu ya kuasi kwao na kuyafanyia uadui kwao mambo Aliyoyatukuza Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net