Al-Maaida 5:77
المائدةقُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَا تَغْلُوا۟ فِى دِينِكُمْ غَيْرَ ٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓا۟ أَهْوَآءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا۟ مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا۟ كَثِيرًا وَضَلُّوا۟ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Wala msifuate matamanio ya kaumu waliokwishapotea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Wala msifuate matamanio ya watu walio kwisha potea tangu zamani, na wakawapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa. [77]
[77] Ewe Mtume! Waambie Watu wa Kitabu, yaani Mayahudi na Wakristo: Mwenyezi Mungu anakukatazeni msivuke mipaka katika itikadi zenu hata mkaingia katika upotovu, mkawafanya baadhi ya viumbe vyake kuwa ni miungu; au mkakanusha ujumbe wa baadhi ya Mitume. Na anakukatazeni kufuata matamanio ya watu walio kutangulieni, walio acha njia ya uwongofu, na wakawazuia watu wengi kuifuata njia hiyo, na wakaendelea katika kuiepuka Njia ya Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Wanaswara, Msiikiuke haki katika yale mnayoyaamini kuhusu mambo ya al-Masîḥ. Wala msifuate matamanio yenu kama Mayahudi walivyofuata matamanio yao katika mambo ya dini, wakaingia kwenye upotevu, wakawafanya watu wengi wamkanushe Allah Mtukufu na wakatoka kwenye njia nyofu, wakaifuata njia ya upotovu na upotevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net