Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 76

Al-Maaida 5:76

المائدة

قُلْ أَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَمْلِكُ لَكُمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا ۚ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلْعَلِيمُ

Maana

Sema: Je, mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawamilikii kudhuru wala kunufaisha? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia vyema, Mwenye kujua yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Je! Mnawaabudu, badala ya Mwenyezi Mungu, wale ambao hawawezi kukudhuruni wala kukufaeni? Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kujua. [76]

[76] Ewe Mtume! Waambie hawa wapotovu: Vipi mnamuabudu mungu asiye weza kukudhuruni kwa lolote mkiacha kumuabudu, wala hawezi kukufaeni kwa lolote mkimuabudu!! Vipi mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu ambaye Yeye ndiye Mungu Mwenye uweza wa kila kitu, naye ni Mwenye kusikia, na Mwenye ujuzi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, ewe Mtume, kuwaambia makafiri hawa, «Vipi mtamshirikisha Allah Mtukufu na asiyeweza kuwadhuru chochote wala kuwaletea manufaa yoyote?» Allah Mtukufu Ndiye Mwenye kuyasikia maneno ya waja Wake, Ndiye Mwenye kuzijua hali zao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net