Al-Maaida 5:75
المائدةمَّا ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ ٱلرُّسُلُ وَأُمُّهُۥ صِدِّيقَةٌ ۖ كَانَا يَأْكُلَانِ ٱلطَّعَامَ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُبَيِّنُ لَهُمُ ٱلْـَٔايَـٰتِ ثُمَّ ٱنظُرْ أَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ
Masihi mwana wa Maryam si chochote isipokuwa ni Mtume. Wamekwishapita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyowabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyogeuzwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Masihi mwana wa Maryam si chochote ila ni Mtume. Wamekwisha pita Mitume kabla yake. Na mama yake ni mwanamke mkweli. Wote wawili walikuwa wakila chakula. Angalia jinsi tunavyo wabainishia Aya, kisha angalia vipi wanavyo geuzwa. [75]
[75] Isa bin Maryamu si chochote ila ni mwanaadamu aliye pata neema ya Mwenyezi Mungu kwa kuteuliwa kuwa ni Mtume kama walivyo mtangulia wengi kabla yake. Na Mama yake Isa ni mmoja katika wanawake, aliye jaaliwa kuwa ni mkweli katika kauli yake na mwenye kumuamini Mola wake Mlezi. Na yeye na mwanawe, Isa, walikuwa wana mahitajio yanayo hitajiwa na kila mwanaadamu, kama kula na kunywa, na kwenda haja. Na hizo ni dalili za ubinaadamu wao. Basi hebu zingatia, ewe mwenye kusikia, hali ya hao walio ingia upofu hata hawaoni dalili za Ishara zilizo wazi ambazo amewabainishia Mwenyezi Mungu. Tena zingatia vipi wanaiacha Haki juu ya kuwa ni iwazi kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuwa al-Masîh, mwana Maryam isipokuwa ni Mtume kama wale Mitume waliomtangulia; na mamake aliamini Imani ya dhati, kiilimu na kivitendo. Na wote wawili wanahitajia chakula kama walivyo binadamu wengineo. Na anayehitaji chakula ili aishi, hawi ni mungu. Basi izingatie, ewe Mtume, hali ya hawa makafiri.Tumekufafanulia alama zinazoonyesha upweke wetu na ubatilifu wa yale wanayoyadai kuhusu Mitume wa Allah Mtukufu. Kisha wao, pamoja na hilo, wanapotea njia ya haki ambayo sisi tunawaongoza waifuate. Kisha hebu angalia, vipi wanaepushwa na haki baada ya ufafanuzi huu?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net