Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 74

Al-Maaida 5:74

المائدة

أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى ٱللَّهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Je, hawatubii kwa Mwenyezi Mungu na wakamwomba awafutie dhambi? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawatubu kwa Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha? Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira na Mwenye kurehemu. [74]

[74] Je! Watu hawa hawaziachilii mbali hizo itikadi za uzushi na uwongo, wakarejea kwenye Imani ya Mwenyezi Mungu, na wakaomba wafutiwe dhambi zao walizo zitenda? Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu wa maghfira, Mwingi wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mbona Wanaswara hawa hawarudi kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na wakatubia kwa waliyoyasema na wakamuomba msamaha Allah Mtukufu? Kwani Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mwenye kuyasamehe madhambi ya wenye kutubia, ni Mwenye huruma kwao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net