Al-Maaida 5:73
المائدةلَّقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ ثَالِثُ ثَلَـٰثَةٍ ۘ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّآ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۚ وَإِن لَّمْ يَنتَهُوا۟ عَمَّا يَقُولُونَ لَيَمَسَّنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ مِنْهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Hakika, wamekufuru wale waliosema: 'Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa watatu.' Hali hakuna mungu isipokuwa Mungu Mmoja tu. Na ikiwa hawayaachi hayo wanayoyasema, basi kwa yakini itawagusa wale waliokufuru miongoni mwao adhabu chungu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwa hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni wa tatu wa Utatu. Hali hakuna mungu ila Mungu Mmoja. Na ikiwa hawaachi hayo wanayo yasema, kwa yakini itawakamata adhabu chungu wale wanao kufuru. [73]
[73] Haiwi mwenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu ni mmoja katika Utatu, kama wadaivyo Wakristo sasa, awe anamuamini Mwenyezi Mungu.!! Na hakika iliyo thibiti ni kuwa hapana mungu ila Mwenyezi Mungu mmoja pekee. Na ikiwa hawa walio potoka hawatoacha itikadi zao potovu, wakarejea kwenye ut'iifu wa Mwenyezi Mungu, hapana budi ila itawasibu adhabu kali. (Biblia inasema kuwa ya kwanza katika Amri Kumi alizo pewa Musa ni: "Usiwe na miungu mingine ila mimi." - Kutoka 20.3. "Wewe umeonyeshwa haya, ili upate kujua ya kuwa Bwana ndiye Mungu, hapana ila yeye." - Kumbukumbu la Torati 4.35. Katika Injili ya Yohana 17.3 Yesu anamsemeza Mwenyezi Mungu: "Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.")
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wamekufuru Wanaswara waliosema, «Allah Mtukufu ni mkusanyiko wa vitu vitatu: Baba, Mwana na Roho mtakatifu.» Kwani Wanaswara hawa hawakujua kwamba watu hawana isipokuwa muabudiwa Mmoja, Hakuzaa wala Hakuzaliwa? Na iwapo wenye kusema maneno haya hawatakoma na uzushi wao na urongo wao, hakika itawapata wao adhabu iliyo kali iumizayo kwa sababu ya kumkufuru kwao Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net