Al-Maaida 5:72
المائدةلَقَدْ كَفَرَ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْمَسِيحُ ٱبْنُ مَرْيَمَ ۖ وَقَالَ ٱلْمَسِيحُ يَـٰبَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ ٱعْبُدُوا۟ ٱللَّهَ رَبِّى وَرَبَّكُمْ ۖ إِنَّهُۥ مَن يُشْرِكْ بِٱللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ ٱللَّهُ عَلَيْهِ ٱلْجَنَّةَ وَمَأْوَىٰهُ ٱلنَّارُ ۖ وَمَا لِلظَّـٰلِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ
Hakika, wamekufuru wale waliosema: 'Hakika, Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryam!' Na hali Masihi mwenyewe alisema: 'Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani, mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu amemharamishia Bustani ya mbinguni, na pahali pake ni Motoni. Na madhalimu hawatakuwa na wowote wa kuwanusuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika wamekufuru walio sema: Mwenyezi Mungu ni Masihi mwana wa Maryamu! Na hali Masihi mwenyewe alisema: Enyi Wana wa Israili! Muabuduni Mwenyezi Mungu, Mola wangu Mlezi na Mola wenu Mlezi. Kwani anaye mshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharimishia Pepo, na mahala pake ni Motoni. Na walio dhulumu hawatakuwa na wa kuwanusuru. [72]
[72] Wenye kudai kuwa Mwenyezi Mungu yu katika Isa bin Maryam hata akawa yeye Mungu, kama wasemavyo Wakristo hii leo, hakika wamekufuru! Yeye Isa hana dhambi ya haya, kwani hakupata kudai hivyo hata mara moja. Bali yeye aliwaamrisha Wana wa Israili wamsafie imani Mwenyezi Mungu peke yake kwa kusema: Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye niumba mimi na nyinyi, na ndiye anaye niendeshea mambo yangu yote, na kwamba kila mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu malipo yake ni kuwa hatoingia Peponi kabisa, bali ataingia Motoni, kwa kuwa amekiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kuvunja mipaka yake hataepuka na adhabu.(Yesu kasema: "Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu ni Bwana mmoja." Marko 12.28. "Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe".Yohana 5.30 "Ninapaa kwenda kwa...Mungu wangu naye ni Mungu wenu." Yohana 20.17 )
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anaapa kwamba wale ambao walisema, «Allah Mtukufu Ndiye al-Masîh, mwana wa Maryam,» wameshakufuru kwa maneno yao haya. Na Alitoa habari Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kwamba al- Masîh, alisema kuwaambia Wana wa Isrãîl, «Muabuduni Allah Mtukufu, Peke Yake, Asiye na mshirika, kwani mimi na nyinyi katika uja tuko sawa.» Kwa hakika, yoyote atakayemuabudu mwingine, pamoja na Allah Mtukufu, Aliye Pweke, basi Allah Mtukufu Ataifanya Pepo kuwa ni haramu kwake na Ataufanya Moto kuwa ndio makao yake na hatakuwa na msaidizi wa kumuokoa nao Moto huo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net