Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 71

Al-Maaida 5:71

المائدة

وَحَسِبُوٓا۟ أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا۟ وَصَمُّوا۟ ثُمَّ تَابَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا۟ وَصَمُّوا۟ كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِمَا يَعْمَلُونَ

Maana

Na wakadhani kuwa hapatakuwa majaribio; basi wakawa vipofu na viziwi. Kisha Mwenyezi Mungu akawapokelea toba zao. Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona vyema hayo wayatendayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wakadhani kuwa hapatakuwa majaribio; basi wakawa vipofu na viziwi. Kisha Mwenyezi Mungu akawapokelea toba zao. Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona hayo wayatendayo. [71]

[71] Na hao Wana wa Israili walidhani hawatapata majaribio, yaani shida za kuwafafanua baina ya walio simama imara na wasio simama imara. Kwa hivyo hawakuweza kustahamili, bali wengi wao walipotea wakawa kama vipofu na viziwi. Wakaiacha Haki, na Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa madhila. Baadae walipo rejea kwa Mwenyezi Mungu na wakatubu, alikubali toba zao, na akawarejeshea utukufu wao. Lakini baadae tena wakaingia katika upotofu, na wakawa kama vipofu na viziwi! Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema, na atashuhudia vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na walidhania waasi hawa kwamba Allah Mtukufu Hatawatia mkononi kwa kuwaadhibu kwa sababu ya kuasi kwao na kutakabari kwao, ndipo wakaendelea katika matamanio yao na wakawa vipofu wa kutouona uongofu na wakawa viziwi wa kutoisikia na kutonufaika na haki. Hapo Allah Mtukufu Aliwateremshia adhabu Yake, wakatubia na Allah Mtukufu Akawakubalia toba zao. Kisha wengi wao walikuwa vipofu na viziwi baada ya kubainikiwa na haki. Na Allah Mtukufu ni Mwenye kuyaona matendo yao, mazuri na mabaya, na Atawalipa kwa matendo yao hayo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net