Al-Maaida 5:70
المائدةلَقَدْ أَخَذْنَا مِيثَـٰقَ بَنِىٓ إِسْرَٰٓءِيلَ وَأَرْسَلْنَآ إِلَيْهِمْ رُسُلًا ۖ كُلَّمَا جَآءَهُمْ رَسُولٌۢ بِمَا لَا تَهْوَىٰٓ أَنفُسُهُمْ فَرِيقًا كَذَّبُوا۟ وَفَرِيقًا يَقْتُلُونَ
Hakika, tulichukua agano la Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipowajia Mtume kwa yale zisiyoyapenda nafsi zao, wengine wao waliwakanusha, na wengine wao wakawaua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tulifanya agano na Wana wa Israili, na tukawatumia Mitume. Kila alipo wajia Mtume kwa wasio yapenda nafsi zao wengine waliwakanusha na wengine wakawauwa. [70]
[70] Sisi tuliagana na Mayahudi, Wana wa Israili, kwa agano madhubuti katika Taurati kuwa wafuate hukumu zake. Na tukawapelekea Manabii wengi wawabainishie, na wawatilie mkazo ahadi yetu. Lakini walivunja ahadi.Wakawa kila akiwajia Mtume ambaye hakuwafikiana na matamanio yao, ama walimkanusha au walimuuwa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika tulichukuwa ahadi ya mkazo kwa Wana wa Isrãîl katika Taurati kuwa watasikia na watatii na tukawapelekea kwa ahadi hiyo Mitume wetu. Lakini walivunja ile ahadi iliyochukuliwa kwao, wakafuata matamanio yao na wakawa kila akiwajia Mtume, miongoni mwa hao Mitume, kwa yale ambayo nafsi zao haziyataki, wanamfanyia uadui: wakawakanusha baadhi yao na wakawaua wengine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net