Al-Maaida 5:69
المائدةإِنَّ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱلَّذِينَ هَادُوا۟ وَٱلصَّـٰبِـُٔونَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ مَنْ ءَامَنَ بِٱللَّهِ وَٱلْيَوْمِ ٱلْـَٔاخِرِ وَعَمِلَ صَـٰلِحًا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Hakika wale walioamini, na Mayahudi, na Masabii na Wakristo, mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya Mwisho, na akatenda mema, basi hawatakuwa na hofu juu yao wala hawatahuzunika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika walio amini, na Mayahudi na Masabii na Wakristo, walio muamini Mwenyezi Mungu, na Siku ya mwisho, na wakatenda mema, basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika. [69]
[69] Hakika walio muamini Mwenyezi Mungu (yaani Waislamu), na wafwasi wa Musa katika Mayahudi, na walio toka kwenye dini nyenginezo, na wafwasi wa Isa katika Manasara - wote hao wakisafisha imani yao kwa Mwenyezi Mungu, na wakaamini kufufuliwa na malipo na wakatenda mema kama ilivyo funzwa na Uislamu, hao wote watasalimika na adhabu na watakuwa katika furaha ya Peponi Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika wale walioamini (nao ni Waislamu), Mayahudi na al-Ṣãbiûn (Masabai, nao ni watu waliosalia kwenye umbile lao na hawana dini fulani waifuatayo), Wanaswara (nao ni wafuasi wa al-Masîḥ), waliomuamini Allah Mtukufu miongono mwao Imani kamilifu, nayo ni kumpwekesha Allah Mtukufu, kumuamini Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na yale aliyokuja nayo, wakaiyamini Siku ya Mwisho na wakatenda matendo mema, basi hao hawatakuwa na hofu yoyote juu ya janga la Siku ya Kiyama wala wao hawatakuwa na huzuni juu ya yale waliyoyaacha nyuma yao duniani.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net