Al-Maaida 5:68
المائدةقُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَىْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَـٰنًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Sema: 'Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muisimamishe Taurati na Injili na yote mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi.' Na hakika uliyoteremshiwa wewe kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie kaumu ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Hamna lenu jambo mpaka muishike Taurati na Injili na yote mlio teremshiwa kutokana na Mola wenu Mlezi. Na hakika ulio teremshiwa wewe kutokana na Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie watu makafiri. [68]
[68] Ewe Mtume! Waambie Watu wa Kitabu (yaani Biblia): Hakika nyinyi hamtakuwa mnafuata Dini sahihi ila mtapo zitangaza hukumu zote za Taurati na Injili na mkazitenda. Na mkaiamini Qur'ani iliyo teremshwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kwa ajili ya kuwaongoa watu. Na yakinika, ewe Mtume, kwamba wengi wa Watu wa Kitabu watazidi udhalimu, na ukafiri, na inadi, juu ya Qur'ani kwa uhasidi wao na chuki. Basi usiwahuzunikie watu ambao wametiwa muhuri wa upinzani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Sema, ewe Mtume, kuwaambia Mayahudi na Wanaswara, «Nyinyi hamuna fungu lolote la dini, madhali hamkuyafuata kivitendo yaliyomo ndani ya Taurati na Injili na Qur’ani aliyokuja nayo Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,» Na hakika wengi wa wale waliopewa Kitabu, haiwaongezei kuteremshiwa wewe Qur’ani isipokuwa ni ujabari na kukanusha. Kwa hivyo, wao wanakuhusudu kwa kuwa Allah Mtukufu Amekutuma kwa ujumbe huu wa mwisho, ambao Ameeleza humo aibu zao. Basi usiwe na huzuni, ewe Mtume, juu ya kule kukukanusha kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net