Al-Maaida 5:67
المائدةيَـٰٓأَيُّهَا ٱلرَّسُولُ بَلِّغْ مَآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ وَإِن لَّمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ يَعْصِمُكَ مِنَ ٱلنَّاسِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ
Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hufanyi, basi hutakuwa umefikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda kutokana na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu ya makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri. [67]
[67] Ewe uliye tumwa na Mwenyezi Mungu! Waeleze watu yote uliyo funuliwa na Mola wako Mlezi, na waite wafuate huo ujumbe, wala usiogope maudhi ya yeyote. Na ukitofanya hivyo basi imekuwa hukufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Kwani wewe umekalifishwa ufikishe ujumbe kwa watu wote. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na maudhi ya makafiri. Ni mtindo wake Mwenyezi Mungu kuwa hamnusuru aliye potea akaiacha Haki. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi makafiri kwenye Njia iliyo kaa sawa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ewe Mtume, fikisha wahyi wa Allah Mtukufu uliyoteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako. Na iwapo utapunguza bidii katika kuufikisha, ukaficha chochote katika wahyi huo, basi utakuwa hukuufikisha ujumbe wa Mola wako. Na kwa hakika, Mtume, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, alifikisha ujumbe wa Mola wake kikamilifu. Basi yoyote atakayedai kuwa yeye alificha chochote, katika yale aliyoteremshiwa, atakuwa amemzulia Allah Mtukufu na Mtume Wake urongo mkubwa. Na Allah Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mwenye kukulinda na kukuokoa na maadui zako. Si juu yako lolote isipokuwa ni kufikisha. Kwa hakika Allah Mtukufu hamuelekezi kwenye uongofu aliyepotea njia ya haki na akayapinga uliyokuja nayo kutoka kwa Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net