Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 66

Al-Maaida 5:66

المائدة

وَلَوْ أَنَّهُمْ أَقَامُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِم مِّن رَّبِّهِمْ لَأَكَلُوا۟ مِن فَوْقِهِمْ وَمِن تَحْتِ أَرْجُلِهِم ۚ مِّنْهُمْ أُمَّةٌ مُّقْتَصِدَةٌ ۖ وَكَثِيرٌ مِّنْهُمْ سَآءَ مَا يَعْمَلُونَ

Maana

Na lau kuwa wangeliisimamisha Taurati na Injili na yote waliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wao Mlezi, basi hakuna shaka wangelikula kutokea juu yao na kutokea chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayoyafanya ni mabaya mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa wangeli ishika Taurati na Injili na yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, basi hapana shaka wangeli kula vya juu yao na vya chini ya miguu yao. Wapo watu miongoni mwao walio sawa, lakini wengi wao wanayo yafanya ni mabaya mno. [66]

[66] Na lau kuwa wao wamezihifadhi Taurati na Injili kama zilivyo teremshwa, na wakazitenda, na wakaamini yote waliyo teremshiwa kutokana na Mola wao Mlezi, nayo ni Qur'ani, Mwenyezi Mungu angeli wakunjulia riziki ikiwajia kutoka kila upande. Na wao si wote sawa katika upotovu. Miongoni mwao, wapo jamaa walio waadilifu, wana akili zao timamu. Hao ndio wale walio muamini Muhammad na wakaiamini Qur'ani. Lakini wengi wao wanatenda vitendo viovu, na wanasema mabaya, na wanajitenga na haki.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau kama wao wangaliyatekeleza yaliyomo ndani ya Taurati na Injili na yale uliyoteremshiwa wewe, ewe Mtume, nayo ni Qur’ani, wangalipata riziki kutoka kila njia: tukawateremshia mvua na kuwaoteshea matunda. Na haya ni malipo ya duniani. Na kwa hakika, miongoni mwa watu waliopewa Kitabu, lipo kundi la wastani lililojikita kwenye haki. Na wengi kati yao, vitendo vyao ni viovu na wamepotea njia ya sawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net