Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 65

Al-Maaida 5:65

المائدة

وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّقَوْا۟ لَكَفَّرْنَا عَنْهُمْ سَيِّـَٔاتِهِمْ وَلَأَدْخَلْنَـٰهُمْ جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ

Maana

Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeliamini na wakamcha Mungu, hapana shaka tungeliwafutia mabaya yao, na tungeliwaingiza katika Mabustani yenye neema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau kuwa Watu wa Kitabu wangeli amini na wakachamungu hapana shaka tungeli wafutia makosa yao, na tungeli waingiza katika Bustani zenye neema. [65]

[65] Na lau kuwa Watu wa Kitabu, yaani Mayahudi na Wakristo, wangeli uamini Uislamu na Nabii wake, na wakaacha madhambi tuliyo yataja, tungeli wafutia makosa yao, na tungeli watia katika Bustani (Pepo) za neema, wakastarehe humo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Lau kama Mayahudi na Wanaswara wangalimuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake, wakazifuata amri Zake na kuyaepuka makatazo Yake, tungaliwafutia madhambi yao na tungaliwatia kwenye mabustani ya Pepo ya starehe katika Nyumba ya Akhera.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net