Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 80

Al-Maaida 5:80

المائدة

تَرَىٰ كَثِيرًا مِّنْهُمْ يَتَوَلَّوْنَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ۚ لَبِئْسَ مَا قَدَّمَتْ لَهُمْ أَنفُسُهُمْ أَن سَخِطَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ وَفِى ٱلْعَذَابِ هُمْ خَـٰلِدُونَ

Maana

Utawaona wengi miongoni mwao wanafanya urafiki wandani na wale waliokufuru. Hakika ni maovu mno ziliyozitanguliza nafsi zao hata Mwenyezi Mungu akawakasirikia, nao watadumu katika adhabu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Utawaona wengi wao wanafanya urafiki na walio kufuru. Hakika ni maovu yaliyo tangulizwa na nafsi zao hata Mwenyezi Mungu amewakasirikia, nao watadumu katika adhabu. [80]

[80] Utawaona wengi miongoni mwa Wana wa Israili hufanya urafiki na washirikina, mapagani, na wanawafanya hao ndio wenzi wao wakishirikiana katika kuupiga vita Uislamu! Kitendo hichi kiovu wanajirimbikizia wenyewe nafsi zao, waje kupata malipo yake kwa kupata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wapate kudumu milele katika adhabu ya Jahannamu.(Hayo yalikuwa zama za Mtume s.a.w. na mpaka hii leo. Mayahudi wanatafuta kila rafiki ambaye atauvunja Uislamu, ilhali yafaa wawaone Waislamu ndio wa karibu mno nao, kwa kuwa wanaamini Mungu Mmoja na wanaamini Manabii wao wote.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Utawaona, ewe Mtume, wengi wa hawa Mayahudi wanawafanya washirikina kuwa ni wategemewa wao. Ni baya mno hilo walilolifanya la mshikamano huo uliokuwa ni sababu ya kukasirikiwa kwao na Allah Mtukufu na kukaa kwao milele kwenye adhabu ya Allah Mtukufu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net