Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 81

Al-Maaida 5:81

المائدة

وَلَوْ كَانُوا۟ يُؤْمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلنَّبِىِّ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْهِ مَا ٱتَّخَذُوهُمْ أَوْلِيَآءَ وَلَـٰكِنَّ كَثِيرًا مِّنْهُمْ فَـٰسِقُونَ

Maana

Na lau wangelikuwa wanamwamini Mwenyezi Mungu, na Nabii huyu, na yale yaliyoteremshwa kwake, wasingeliwafanya hao kuwa marafiki wandani. Lakini wengi miongoni mwao ni wapitao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na lau wangeli kuwa wanamuamini Mwenyezi Mungu, na huyu Nabii, na yaliyo teremshwa kwake, wasingeli wafanya hao marafiki. Lakini wengi katika wao ni wapotofu. [81]

[81] Na lau kuwa itikadi yao ni sawa kama inavyo faa iwe kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, na Mtume wake Muhammad s.a.w., na Qur'ani aliyo teremshiwa, basi wasingeli wafanya makafiri kuwa ni wenzao kuwapinga Waumini. Lakini wengi miongoni mwa Wana wa Israili ni maasi, wameacha dini.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na lau hawa Mayahudi ambao wanasaidiana na washirikina wangekuwa wamemuamini Allah Mtukufu, Aliyetukuka, na Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakayakubali yale yaliyoteremshwa kwake, nayo ni Qur’ani tukufu, hawangaliwafanya makafiri kuwa ni marafiki na waokozi. Lakini wengi katika wao wako nje ya twaa ya Allah Mtukufu na Mtume Wake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net