Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 82

Al-Maaida 5:82

المائدة

لَتَجِدَنَّ أَشَدَّ ٱلنَّاسِ عَدَٰوَةً لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلَّذِينَ أَشْرَكُوا۟ ۖ وَلَتَجِدَنَّ أَقْرَبَهُم مَّوَدَّةً لِّلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ ٱلَّذِينَ قَالُوٓا۟ إِنَّا نَصَـٰرَىٰ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّ مِنْهُمْ قِسِّيسِينَ وَرُهْبَانًا وَأَنَّهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ

Maana

Hakika utawakuta walio na uadui mkubwa mno kuliko watu wote juu ya wale walioamini ni Mayahudi na wale walioshirikisha. Na hakika utawakuta wale wao walio karibu mno kwa mapenzi kwa wale walioamini ni wale waliosema: 'Hakika Sisi ni Manasara.' Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwamba wao hawafanyi kiburi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika utawakuta walio shadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walio amini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta walio karibu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi. [82]

[82] Ewe Nabii! Tunakuhakikishia ya kwamba utaona hapana watu wanao kuchukia na kukubughudhi wewe na wanao kuamini kama Mayahudi na hawa wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu katika ibada. Na utawakuta walio karibu mno nawe kwa mapenzi ni wafwasi wa Isa, walio jiita wenyewe "Manasara". Kwa sababu wamo miongoni mwao makasisi wanao ijua dini yao, na marahibu (mamonaki) wat'awa, wanao mcha Mola Mlezi, na kuwa wao hawana kiburi cha kuwazuia wasisikie Haki. (Na haya yameonakana kuwa Waislamu wengi duniani asili yao walikuwa Manasara, Wakristo. Wao wakisha pata fursa ya kuufahamu Uislamu huufuata, lakini ni wachache miongoni mwa Mayahudi walio silimu. Kinacho wazuia ni kiburi. Lakini walio silimu basi wamekuwa Waislamu wakubwa.)

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Utakuta tena utakuta, ewe Mtume, kwamba watu wenye uadui mno kwa wale waliokukubali wakakuamini na wakakufuata ni Mayahudi, kwa sababu ya ukaidi wao, ukanushaji wao na kuichukia kwao haki, na wale wanaomshirikisha Allah Mtukufu na kitu kingine, kama wanaoabudu masanamu na wengineo. Na utakuta tena utakuta kwamba walio karibu mno kimapenzi na Waislamu ni wale waliosema, «Sisi ni Wanaswara.» Hilo ni kwamba miongoni mwao kuna wasomi wanaoijua dini yao, wacha-Mungu, wanaofanya jitihadi ya ibada kwenye mindule, na kwamba wao ni wanyenyekevu, hawafanyi kiburi cha kukataa haki. Hao ndio wale walioukubali ujumbe wa Mtume Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakauamini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net