Al-Maaida 5:83
المائدةوَإِذَا سَمِعُوا۟ مَآ أُنزِلَ إِلَى ٱلرَّسُولِ تَرَىٰٓ أَعْيُنَهُمْ تَفِيضُ مِنَ ٱلدَّمْعِ مِمَّا عَرَفُوا۟ مِنَ ٱلْحَقِّ ۖ يَقُولُونَ رَبَّنَآ ءَامَنَّا فَٱكْتُبْنَا مَعَ ٱلشَّـٰهِدِينَ
Na wanaposikia yale yaliyoteremshwa kwa Mtume, utayaona macho yao yanamiminika machozi kwa sababu ya haki waliyoitambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanaoshuhudia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
NA WANAPO SIKIA yaliyo teremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachururika machozi kwa sababu ya Haki waliyo itambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanao shuhudia. [83]
[83] Na pia miongoni mwa Manasara wakiisikia Qur'ani aliyo teremshiwa Mtume huathirika nayo, macho huwatiririka machozi, kwa kuwa wanajua kuwa wanayo yasikia ni kweli tupu, basi nyoyo zao humili kwayo, na ndimi zao huomba dua kumwomba Mwenyezi Mungu kwa kusema: Mola wetu Mlezi! Tumekuamini Wewe na Mitume wako, na Haki ulio wateremshia. Basi ipokee Imani yetu, na utufanye miongoni mwa Umma wa Muhammad ulio wafanya mashahidi na hoja kwa watu wote Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na miongoni mwa yale yanayoonyesha mapenzi yao kwa Waislamu ni kuwa kundi katika wao (nao ni tume ya watu wa Habashah walipoisikia Qur’ani) yalibubujika machozi macho yao wakawa na yakini kuwa hiyo ni haki iliyoteremshwa kutoka kwa Allah Mtukufu, Aliyetukuka, wakamuamini Allah Mtukufu, wakamfuata Mtume Wake na wakanyenyekea kwa Allah Mtukufu wakimuomba awatukuze kwa heshima ya kushirikiana na umati wa Muhammad, amani imshukie, katika kuwatolea ushahidi umma wengine Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net