Al-Maaida 5:84
المائدةوَمَا لَنَا لَا نُؤْمِنُ بِٱللَّهِ وَمَا جَآءَنَا مِنَ ٱلْحَقِّ وَنَطْمَعُ أَن يُدْخِلَنَا رَبُّنَا مَعَ ٱلْقَوْمِ ٱلصَّـٰلِحِينَ
Na kwa nini tusimwamini Mwenyezi Mungu na haki iliyotujia, na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na kaumu ya walio wema?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa nini tusimuamini Mwenyezi Mungu na Haki iliyo tujia, na hali tunatumai Mola wetu Mlezi atuingize pamoja na watu wema? [84]
[84] Na nini cha kutuzuia tusimsadiki Mwenyezi Mungu peke yake, na Haki iliyo teremka kwa Muhammad? Na hali sisi tunamtaraji Mwenyezi Mungu atuingize Peponi pamoja na watu wenye Imani njema na vitendo vyema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na walisema, «Kwani tuna lawama gani sisi kwa kumuamini kwetu Allah Mtukufu, kuikubali haki ambayo alikuja nayo kwetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kutoka kwa Allah Mtukufu na kumfuata kwetu yeye, na hali tunatumai kuwa Mola wetu Atatutia kwenye Pepo Yake, Siku ya Kiyama, pamoja na walio watiifu Kwake?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net