Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 85

Al-Maaida 5:85

المائدة

فَأَثَـٰبَهُمُ ٱللَّهُ بِمَا قَالُوا۟ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ خَـٰلِدِينَ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَآءُ ٱلْمُحْسِنِينَ

Maana

Basi Mwenyezi Mungu akawalipa kwa yale waliyoyasema, Mabustani yapitayo mito kwa chini yake, wadumu humo. Na hayo ndiyo malipo ya wafanyao wema.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi Mwenyezi Mungu atawalipa, kwa yale waliyo yasema, Bustani zipitazo mito katika yake; humo watadumu. Na haya ndiyo malipo ya wafanyao wema. [85]

[85] Kwa hivyo Mwenyezi Mungu amewaandikia malipo kwa vile kuungama kwao, nayo ni Bustani yenye kupita mito chini ya miti yake, na majumba ya fakhari ya kukaa humo daima, pamoja na watu ambao ni njema itikadi zao na vitendo vyao.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Akawalipa, kwa waliyoyasema ya kujienzi kwa kuuamini kwao Uislamu na kutaka kwao kuwa pamoja na watu wema, mabustani ya Pepo ambayo, chini ya miti yake inapita mito, hali ya kukaa humo, hawatatolewa humo wala hawatahamishwa. Hayo ndiyo malipo ya wema wao wa maneno na vitendo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net