Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 86

Al-Maaida 5:86

المائدة

وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ

Maana

Na wale waliokufuru na wakazikadhibisha ishara zetu, hao ndio watu wa Jahiim.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale walio kufuru na wakazikanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni. [86]

[86] Na walio mpinga Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wakazikanya dalili alizo wateremshia kuwa ni uwongofu wa kufikia Haki, ni wao peke yao wanao stahiki adhabu kali katika Jahannamu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale ambao waliukanusha upweke wa Allah Mtukufu, wakaukataa unabii wa Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na wakazikanusha aya Zake zilizoteremshwa kwa Mitume Wake, hao ndio watu wa Motoni wenye kukaa daima humo.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net