Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 5 · Aya ya 87

Al-Maaida 5:87

المائدة

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُحَرِّمُوا۟ طَيِّبَـٰتِ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُعْتَدِينَ

Maana

Enyi mlioamini! Msiviharamishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu, wala msivuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipaka.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Enyi mlio amini! Msiharimishe vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msikiuke mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wakiukao mipaka. [87]

[87] Enyi mlio amini! Msijiharimishie nafsi zenu vitu vizuri alivyo kuhalalishieni Mwenyezi Mungu, wala msipite mipaka aliyo kuwekeeni Mwenyezi Mungu ya kufuata mambo ya wastani. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi watu wanao pindukia mipaka.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Enyi ambao mliamini, msiharamishe vizuri alivyowahalalishia Allah Mtukufu, miongoni mwa vyakula na vinywaji na kuoa wanawake, mkayatia mkazo mambo ambayo Allah Mtukufu Ameyatolea nafasi kwenu, na msipite mipaka ya vitu alivyoviharamisha Allah Mtukufu. Kwani Allah Mtukufu Hawapendi wenye kupita mipaka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Maaida

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net